​Je, unahitaji msaada wa matibabu sasa hivi?

Piga simu healthdirect kwa 1800 022 222 ili kupata uangalifu wa kimatibabu ya bure na ya haraka kwa matatizo ya kiafya yasiyo dharura. Katika dharura, wakati wote piga simu Sifuri Mara Tatu (000).

Kwenye ukurasa huu

Kuhusu

Huduma za Matunzo ya Haraka zimeanzishwa jimboni New South Wales (NSW) kusaidia kupunguza shinikizo kwa idara za dharura.

Huduma hizi huwapa watu matibabu wanaohitaji haraka kwa ugonjwa au jeraha ambalo si dha​rura, bila kusubiri kwenye idara ya dharura yenye shughuli nyingi.

Huduma hizi nyingi zina wataalamu wa kimatibabu na vifaa vya uchunguzi ikiwa ni pamoja na eksrei, patholojia, na kwa hiyo huweza kutiba hali mbalimbali.

Mifano ya magonjwa au majeraha ambayo kawaida hayajazingatiwa kuwa dharura inajumuisha:

  • mikato midogo
  • miteguko ya kifundo au mivunjiko yaliyoshukiwa
  • majeraha ya mchezo
  • maambukizo madogo
  • maambukizi ya njia ya mkojo (UTIs)
  • majeraha madogo ya moto
  • upele
  • uma za dudu au mnyama
  • kikohozi, mafua au mafua makali
  • mashambulizi madogo ya pumu
  • maumivu ya masikio
  • homa au kuhisi ubaridi.

Ustahiki

Unaweza kustahiki kupata Huduma ya Matunzo ya Haraka ikiwa wewe:

  • ni mkazi anayeishi katika jumuiya iliyopo jimboni ya NSW au karibu mpakani
  • unapata jeraha au ugonjwa papo hapo ambao si dhar​ura
  • unahitaji tiba ya kimatibabu katika saa 2 hadi 12 zijazo; na
  • huwezi kupata miadi na Daktari wako wa Kawaida (GP) au katika vituo vya matibabu vya karibu.

Jinsi ya kufikia

Tafadhali piga simu healthdirect kwa 1800 022 222 bila malipo wakati wowote (saa 24 za siku, siku 7 za wiki).

Muuguzi aliyesajiliwa (RN) atajibu simu yako na atakuuliza maswali kuhusu hali yako.

Kulingana na tathmini ile kufanywa na muuguzi, unaweza kuelekezwa kwa Huduma ya Matunzo ya Haraka.

Ikiwa unaelekezwa kwa Huduma ya Matunzo ya Haraka, muuguzi aliyesajiliwa atakupa maelezo ya kufikia huduma ile.

Kulingana na hali yako, muuguzi aliyesajiliwa anaweza kupendekeza chaguo badala la matibabu kwa ajili yako.

Je, unahitaji msaada wa ziada?

  • Piga simu kwa Huduma ya Utafsiri na Ukalimani (TIS) kwa 131​ 450  kupata usaidizi wa lugha.
  • Wasiliana na National Relay Service kupata usaidizi wa kusikia au kunena.

Ada na malipo

Iwapo umeelekzwa kwa Huduma ya Matunzo ya Haraka, hakutakuwa na gharama zinazohusiana na matibabu yako ikiwa wewe:

  • una kadi halili ya Medicare card; au
  • ni mtafutaji hifadhi anayekaa kwenye jamii.

Ikiwa yoyote hayakuhusu, tafadhali fahamu unaweza kupewa matunzo kwa huduma tofauti na kunaweza kuwa gharama zinazohusiana na matibabu yako.

Ikiwa una matatizo yoyote ya kipesa, healthdirect inaweza kukutoa chaguo la matibabu linalofaa zaidi kwa mazingira yako.

Mahali

Huduma za Matunzo ya Haraka zipo katika

  • Sydney Mji Mzima
  • Illawarra
  • Central Coast
  • Hunter Valley
  • New England
  • Mid North Coast
  • NSW Kaskazini
  • NSW Kusini
  • NSW Magharibi

Huduma za Matunzo ya Haraka zinapatikana pia kupitia simu (telehealth) kama upo nje ya maeneo hayo, au kama muuguzi aliyesajiliwa kwa healthdirect akiamua hii ni chaguo la matibabu lilofaa zaidi kwa ajili yako.

Saa za kufungua

Huduma za Matunzo ya Haraka hufanya kazi kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 2 usiku kila siku, ikiwemo likizo za umma. Vinginevyo, telehealth (huduma ya simu) inapatikana saa 24 ya siku, siku 7 ya wiki.

Ahadi ya serikali

Idara ya Afya ya NSW imeweza kutoa Huduma za Matunzo ya Haraka kwa umma kwa kushukuru usaidizi wa Serikali ya NSW, pamoja na Serikali ya Australia.

Serikali ya NSW imeahidi dola milioni 124 ya ufadhili kwa miaka miwili kutoa Huduma 25 za Matunzo ya Haraka kwenye NSW hadi kati ya mwaka 2025.

Serikali ya Australia imeahidi ufadhili pia kutoa Kliniki za Medicare za Matunzo ya Haraka jimboni NSW.

Nyenzo

Tusaidie kueneza habari kuhusu Huduma za Matunzo ya Haraka kupitia chaneli zako na nyenzo zetu zilizoandaliwa tayari.

Tazama nyenzo

Current as at: Thursday 29 August 2024
Contact page owner: System Purchasing