Monoksidi kaboni ni nini?
Monoksidi kaboni ni gesi yenye hatari. Kuipumua ndani kunaweza kukufanya mgonjwa au hata kukuua.
Ni vigumu kujua kama monoksidi kaboni ipo – huwezi kuiona, kuinusa au kuisikia.
Nani anaweza kuwa mgonjwa kutokana na monoksidi kaboni?
Mtu yeyote anaweza kuwa mgonjwa kutokana na monoksidi kaboni.
Watu wengine wanaweza kuwa wagonjwa zaidi kuliko wengine. Watu hawa ni:
- Watoto wachanga
- Wanawake wajawazito
- Wazee
- Watu wenye magonjwa mengine ya muda mrefu, kama matatizo ya moyo.
Je, monoksidi kaboni inapatikana wapi?
Monoksidi kaboni inatengenezwa na kuchoma mafuta kama:
- Gesi ya asili
- Petroli
- Kuni
- Makaa
- Makaa ya mawe.
Vitu vingi vya kaya vinachoma mafuta hayo na kutengeneza monoksidi kaboni.
Monoksidi kaboni inaweza kukwama ndani nyumbani kwako, haswa wakati milango na madirisha yamefungwa. Hii inaweza kufanya monoksidi kaboni kuongezeka kwa viwango vya hatari.
Je, nitunzaje usalama wangu na wa familia yangu?
Barbeki, grill na hita za nje
Usilete ndani barbeki, grill au hita za nje za gesi katika nyumbani kwako. Hizo ni kutumia nje tu. Vitu hivi vinachoma mafuta kama gesi ya asili, kuni, na makaa (mawe madogo au marefu).
Ikiwa unatumia vitu hivi ndani ya nyumba, monoksidi kaboni inaweza kuongezeka haraka kwa viwango vya hatari.
Angalia vizuri mafunzo ya kitu kuona kama unapaswa kutumia ndani au nje ya nyumba.
Injini ya petroli
Usitumie vitu vyenye injini ya petroli ndani nyumbani kwako au gereji, hata sio na milango na madirisha wazi.
Vitu vingine vinavyokuwa na injini za petrol ni:
- Magari na mashua
- Kifaa cha kuoshea na shinikizo
- Misumeno ya saruji
- Jenereta.
Hita za gesi
Ikiwa unatumia hita ya gesi katika nyumbani kwako:
- Angalia mafunzo hayo kuhakikisha kuwa unaweza kutumia hita ndani ya nyumba.
- Hakikisha kuwa mpiga gesi aliyesajiliwa huangalia hita angalau kila miaka miwili.
- Fikiria kuhusu kuweka kengele ya monoksidi kaboni ili kukuonya ikiwa viwango vinaanza kuzidisha. Kengele ya monoksidi kaboni ni tofauti na kengele ya moshi.
Je, niwekaje kengele ya monoksidi kaboni?
Ikiwa unaamua kuweka kengele ya monoksidi kaboni katika nyumbani kwako, unapaswa kufanya ifuatayo:
- Chagua kengele ya monoksidi kaboni inayosema inaridhi viwango katka USA (UL2034) au Ulaya (EN50291).
- Weka kengele za monoksidi kaboni karibu vyumba vyote vya kulala na vyumba vyenye hita za gesi katika nyumbani kwako.
- Fuata mafunzo kwa kusakinisha, kudumisha na kutumia kengele ya monoksidi kaboni.
Je, nitajuaje kama mtu anaumizwa na monoksidi kaboni?
Inasaidia kufahamu dalili za ugonjwa kutokana na monoksidi kaboni.
Kadiri monoksidi kaboni unavyopumua, ndivyo dalili za ugonjwa zinavyozidi kuwa mbaya.
Kupumua kiasi
kidogo zaidi cha gesi kunaweza kusababisha:
- Kichwa kuumwa
- Kichefuchefu
- Kutapika
- Kujisikia udhaifu.
Kupumua kiasi
kikubwa zaidi cha gesi kunaweza kusababisha:
- Kuhisi kizunguzungu
- Kujisikia kuzimia
- Kupoteza ufahamu
- Jeraha la ubongo wa kudumu na kifo.
Niweze kufanya nini ikiwa nafikiri mtu anaumizwa na monoksidi kaboni?
Ikiwa mtu ana kizunguzungu au anazimia au amepoteza ufahamu, hii ni dharura. Piga simu Sifuri Mara Tatu (000).
Ikiwa mtu ana maumivu ya kichwa, kichefuchefu au anatapika au anahisi udhaifu:
- Toa kila mtu nje ya nyumba na kupuma hewa nzuri ya nje.
- Piga simu kwa Kituo cha Taarifa ya Sumu (Poisons Information Centre) kwa 13 11 26 kupata ushauri wakati wowote.
- Ikiwa unahitaji mkalimani, piga simu kwa TIS kwa 131 450 na uliza kuzungumza na Kituo cha Taarifa ya Sumu.
Kujua zaidi
Angalia tovuti hizi kujifunza zaidi juu ya njia za salama kupasha joto nyumba yako